Thursday, September 1, 2011

WILL SMITH NA JADA PINKETT WAKANUSHA KUVUNJIKA NDOA YAO. JAY LO NA MARC ANTHONY PIA WAZUNGUMZIA YAO.

Tesesi zilizoenea katika pembe mbalimbali za dunia kwamba Muigizaji Sinema na Mwanamuziki maarufu wa nchini Marekani Will Smith (Fresh Prince) ameachana na mkewe Jada Pinkett, zimekanushwa vikali na wanandoa hao kuwa sio za kweli.

 Wanandoa hao mastaa maarufu wamekaririwa wakisema “Ingawa tunasita kuongelea au kujibishana na vyombo vya habari vya aina hii, tetesi zilizoenezwa kuhusu uhusiano wetu sio za ukweli hata kidogo”, walisema wanandoa hao kwa kauli ya pamoja jumanne iliyopita Agosti 23 kufuatia gazeti la InTouch Magazine kutoa taarifa hizo. “Bado tupo pamoja, na ndoa yetu ipo imara” walisikika wanadoa hao wakisisitiza suala hilo.

 Will Smith na Jada Pinkett walifunga ndoa miaka 13 iliyopita wakati wa mkesha wa mwaka mpya wa 1997 huko Baltimeore na wamefanikiwa kupata watoto wawili pamoja, mvulana Jaden (13) na msichana Willow(10).

Aidha Wanamuziki Marc Anthony na Jennifer Lopez (Jay Lo) waliona miaka saba iliyopita na kufanikiwa kupata watoto wawili mapacha wenye umri wa miaka mitatu, wa kiume Max na wakike Emme. Jay Lo na Marc baadaye walitangaza kuachana rasmi kupitia vyombo vya habari lakini tena ilipofika June, 2004 wanandoa hao waliamua kuoana tena kwa siri nyumbani kwao huko Beverly Hill, California.

 Mpambe wa karibu wa Jada, Karynne Tencer amesema kuwa “Zimetoka tetesi nyingi kuhusu Marc Anthony kuachana na Jennifer Lopez na hili la Will kuachana na Jada, zote sio za kweli, ni uongo. Kwa taarifa kuhusu utengano wa Jada na Will, siwezi kutoa maoni yoyote kuhusu maisha yao binafsi”. Mwakilishi wa Marc Antony nae amesema kuwa “Tunaunga mkono kukanusha huku. Yametosha sasa. Kuna familia husika, watoto wanaohusika, urafiki unahusika pia. Hizi habari SIO ZA KWELI.”
Will akiwa na mkewe Jada na watoto wao Jaden na Willol.

Will Smith na Jada Pinkett katika pozi.


Jennifer Lopez akiwa na mumewe Marc Anthony

Jay Lo na Marc Anthony pamoja na twins wao Max na Emme

No comments:

Post a Comment

Unaonaje hii?