Saturday, August 27, 2011

BUNGE LA NNE LA BAJETI LAHITIMISHWA KWA VITUKO DODOMA

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limehitimisha kikao chake cha Nne cha bjaeti ijumaa hii tarehe 26/08/2011 huko mjini Dodoma kwa Wizara mbalimbali kuwasilisha bajeti zake na kujadiliwa ili kupitishwa kwa ajili ya mwaka mpya wa fedha wa serikali wa 2011/2012.

Mchakato wa kikao hicho ulikuwa na vituko pamoja na changamoto nyingi zilizoweza kujitokeza zikiwemo baadhi ya wabunge kutolewa nje ya ukumbi kwa kukiuka taratibu na miongozi ya mkutano, migogoro kuhusu suala la upatikanaji hafifu wa umeme na mafuta ya kuendeshea mitambo (petroli na dizeli) pamoja na suala la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo kushutumiwa kuchangisha pesa kwa wanawizara wake ili kufanikisha kupitisha bajeti ya wizara yake ya Nishati na Madini ipite bila ya kupingwa hali iliyosababisha Bw. Jairo kusimamishwa kwa muda na baadae kurudishwa tena kazini na Bw. Luhanjo, kitendo ambacho kilitafsiriwa kama ni "Kulidharau Bunge".
Suala la Bw. Jairo kurudishwa tena kazini lilileta maneno mengi kwa jamii wa Watanzania wengi hali ambayo pia ilisababisha siku ya jumanne wabunge kutishia kusimamisha shughuli zote za Serikali katika Bunge hilo hadi hapo uchunguzi wa Jairo ambaye alituhumiwa na Mbunge wa Kilindi kuwa anahusika na uchangishaji wa fedha zitakapopelekwa bungeni. Hata hivyo, Rais Kikwete aliamua kumsimamisha kazi Bw. Jairo kwa mara ya pili ili kupisha uchunguzi zaidi juu ya tuhuma zinazomkabili kuhusiana na matumizi mabaya ya madaraka yake.
Spika wa Bunge, Mama Anne Makinda akitoka bungeni mara baada ya kuhitimisha mkutano wa Bajeti 2011/12

Mbunge kijana wa Kisarawe CCM, Bw. Suleiman Jaffo akitoka mjengoni mara baada ya kumalizika kwa kikao cha bajeti cha bunge jijini Dodoma. Wananchi wa Kisarawe kaeni mkao wa kula, maji hayooooooooo!!

NYUSO ZA FURAHA; Bw. Jairo (kushoto) na Waziri wake Bw. Ngeleja mara baada ya kuruhusiwa kurudi kazini kabla ya kusimamishwa tena na Baba Ridhiwani.

Hii ndiyo barua iliyomletea matatizo Bw. Jairo.

Mmmh! Hii ndiyo Tanzania yetu na hili ndilo Bunge letu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.

No comments:

Post a Comment

Unaonaje hii?