Tuesday, September 6, 2011

JOYCE KIRIA AFUNGA NDOA!!!! TENA AU?? WEWE UNAJUA HIYO???

Mtangazaji maarufu wa kituo cha Televisheni cha East Africa Bi. Joyce Kiria amefunga ndoa mapema mwanzoni mwa mwezi huu siku ya jumapili tarehe 04 Septemba, 2011. Ndoa hiyo aliyofunga na Bw. Henry John Kileo ilifuatiwa na hafla fupi iliyofanyika katika hoteli ya Atrium iliyopo Sinza jijini Dar.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na waheshimiwa wabunge wa CHADEMA, Bw. Godbless Lema (Arusha Mjini), Bw. Freeman Mbowe (Hai) na Bw. John Mnyika (Ubungo) pamoja na wadau wengine mbalimbali.

 SINA UHAKIKA ila inasemekana kuwa Bi. Joyce ni mke wa mtu na alishawahi kufunga ndoa (nakumbuka alikuwa anatumia jina la Joyce Kiria Nkongo) lakini sasa hatumii jina hilo na ameolewa na Bw. Henry J. Kileo.
Mimi sio mwanzilishi wa hili ila nimeipata huku, BOFYA HAPA AU ANGALIA HAPA
Bw. Henry J. Kileo akimvisha pete ya ndoa mke wake Bi. Joyce Kiria

Bi. Joyce Kiria akiwa katika pozi la furaha mara baada ya kufunga ndoa.

 Hongera Dada Joyce na Bw. Henry Kileo, Mungu abariki ndoa yenu.

2 comments:

  1. umependeza Joyce nakutakia ndoa yenye baraka na mungu awatangulie

    ReplyDelete
  2. Hongera Joyce and Henry maisha hupangwa na Mungu watu wapo kwa ajili ya kuongea hakuna anayejua kwa nini uliachana na Nkongo,maisha lazima yaendelee jamani watu tusipende kuhukumu tutahukumiwa!!!!!!!!!!!!!!!!!! Mungu awabariki yeye ndiye mwamuzi wa yote usisahau sala mdogo wangu ndiyo mwongozo na majibu ya maswali yoote.

    ReplyDelete

Unaonaje hii?