Thursday, September 1, 2011

BENYONCE AONESHA MIMBA YAKE JUKWAANI

Hivi karibuni, mwanamuziki Beyonce Knowles alisimama jukwani wakati akifanya perfomance ya nyimbo zake katika tamasha aliamua kufungua vifungo vya kikoti chake na kuonesha tumbo la mimba yake huku mumewe Jay Z akifurahia kwa pembeni.

 Yamkini Beyonce aliamua kufanya kituko hicho kufuatia uvumi uliokuwa ukienea kwa miaka kadhaa kuwa mwanamuziki huyo ni mjamzito lakini sasa imethibitika kuwa kweli, kama wahenga walivyosema “Lisemwalo lipo na kama halipo laja” na sasa Beyonce ameamua kuweka bayana suala hilo.

 Beyonce ambaye anatarajia kupata mtoto wake wa kwanza na mumewe ambaye pia ni Mwanamuziki Jay Z ambapo uzao huo unatarajiwa kuwa ni uzao mwema kwao kwani magazeti mengi ya udaku yamekuwa yakiripoti kimakosa kuhusu Beyonce kuwa ni mjamzito mara kwa mara na kuwachanganya wapenzi wa mwanadada huyo.
Kama kuna jambo moja ambalo linaweza kumlamzimisha mrembo wa R&B kuvaa nguo nyepesi za kisasa na za kawaida, ni wakati wa matarajio ya uzazi kwa akinamama ujauzito), ni furaha sana.
Beyonce akitabasamu kwa washabiki wake huku akiwa ameshikilia tumbo lake.
Ili kuona live video ya kituko hicho cha Beyonce; BOFYA HAPA TARTIIIBU.

No comments:

Post a Comment

Unaonaje hii?