Tuesday, August 2, 2011

HUJAFA HUJAUMBIKA!! JAMANI, TUMSAIDIE KIJANA MGUU UNAMSUMBUA SANA

Kijana Abbas akiwa amepumzika nyumbani kwao baada ya kukosa matumaini
 



Kijanaana Abbas Abdalaah (31) mkazi wa Kijiji cha Kiru Ndogo, Wilaya ya Babati mkoani Manyara aliapoanza kuvimba uvimbe mdogo katika mguu wake wa kulia hakujua kuwa ulikuwa ni mwanzo wa ugonjwa ambao hatimaye ungemfanya ashindwe kutembea.Ugonjwa huo ambao mpaka sasa haujulikani, umemfanya Abbas kulala kitandani muda wote akilazimika kubebwa na watu watano kumpeleka nje kujisaidia.

Matumaini aliyokuwa nayo ya kupata tiba ya ugonjwa wake, yameanza kutoweka baada ya msamaria aliyejitokeza kumpeleka Hospitali ya Seliani mjini Arusha kushindwa kutimiza ahadi yake. Kwa habari zaidi juu ya mkasa uliomkumba Kijana Abbas na namna ya kuweza kumsaidia BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment

Unaonaje hii?