Thursday, July 21, 2011

HATIMAYE REPA DMX ATOKA JELA

Repa maarufu wa Marekani DMX ameachiwa huru jana Julai 19, 2011 kutoka katika gereza la Yuma, Arizona alipokuwa anatumikia kifungo cha mwaka mmoja baada yakukaidi kupimwa kiwango cha dawa za kulevya na kusababisha machafuko.  

DMX mara baada ya kuachiwa, alilakiwa na kikundi kidogo cha rafiki zake na akasema kuwa amefurahi sana na kuongeza kuwa safari yake ya kwanza baada ya kutoka jela ataenda kumuona mtoto wake jioni na baada ya hapo ataingia studio.

DMX alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela Desemba 2010 na mpaka anaachiwa huru jana, ameweza kutumikia kifungo hicho kwa muda wa miezi saba tu.
Kwa picha zaidi na video ya maelezo yake wakati akitoka jela BONYEZA HAPA

Repa DMX wakati akiwa jela
DMX mara baada ya kutoka jela mapema jana.

No comments:

Post a Comment

Unaonaje hii?