Wednesday, July 20, 2011

MAONESHO YA MALIASILI SABASABA YAMALIZIKA

Maonesho ya Wanyama na Viumbe hai wa asili yaliyokuwa yakiendeshwa na Wizara ya Maliasili na Utalii yamemalizika rasmi jana tarehe 19/07/2011 katika viwanja vya Mwl. Nyerere (Sabasaba).
Banda la Maonesho la Wizara hiyo lilivutia watu wengi walioshiriki katika maonesho ya Viwanda na Biashara (Sabasaba) hali iliyopelekea watu wengi kushindwa kuingia ndani kuona wanyama kutokana na umati mkubwa wa watu waliofurika wakati wa msimu wa Sabasaba (Julai 01 hadi 07, 2011).
Hata hivyo, watu wengi walioonenda kuangalia wanyama hao baada ya tarehe hizo waliweza kufaidi kuangalia viumbe mbalimbali bila ya malipo yoyote na kwa uhuru bila ya msongamano wa watu.



Bango la Maliasili likikaribisha watalii
Simba akiwa katika pozi.
Mnyama Duma

No comments:

Post a Comment

Unaonaje hii?